Mwongozo wa usimamizi shirikishi unaohusisha jamii ya wavuvi wa pwani ya bahari ya hindi

Mwongozo huu umeandaliwa kwa ajili ya kuanzisha usimamizi shirikishi wa raslimali za pwani na bahari unaohusisha jamii. Kitabu hiki kimeandaliwa kwa ajili ya kuwafundisha waraghabishi na baadae kitumike kutoa mafunzo kwa jamii. Mwongozo huu umegawanyika katika masomo sita ambayo ni Sera na Sheria ya Uvuvi; Usimamizi wa Shughuli za Uvuvi; Usimamizi shirikishi unaohusisha jamii; Utawala bora; Utatuzi wa migogoro na Viashiria. Wakati wa kutoa mafunzo kwa waragabishi ni lazima kufundisha masomo yote sita ili wafahamu maeneo ya msingi. Baada ya mafunzo wahitimu watawaelimisha jamii ya wavuvi ili waanzishe usimamizi shirikishi wa raslimali za pwani na bahari unaohusisha jamii katika vijiji vyao. Pia, wahitimu (waraghabishi) watatakiwa kutumia elimu waliyoipata kuwafundisha Viongozi wa Serikali za Vijiji, Maafisa Watendaji wa Vijiji, Maafisa Watendaji wa Kata na viongozi wengine wa ngazi za Tarafa na Wilaya.
Author: 
Fishery Development Division and WWF
Language: 
Swahili
Document date: 
2009-03